CHRISTINA MATAI (mwang'onda) ni mwanamuziki wa nyimbo za injili aliye anza uimbaji mnamo mwaka 1998 akiwa ni muimbaji katika kundi lililofahamika kwa jina la THE WINNAS, na mnamo mwaka 2004 alitoa albamu yake ya kwanza akiwa nje ya kundi iliyoitwa YESU NI NANI.
christina anaye fahamika kwa jina la THE TANZANITE LADY akiwa ni muasisi wa nyimbo za injili katika maadhi ya taarab, wimbo wake wa kwanza uliojulikana kama UJUMBE KWA WANAWAKE wenye asili ya taarab ulimfanya awe mwanamuziki wakwanza kuimba wimbo wenye maadhi hayo. Christina Matai Huudumu katika sehemu mbalimbali na ikiwemo mikutano, makanisa, semina na hata katika matamasha mbalimbali ya kijamii.
christina matai akiwa kwenye moja ya harusi akiwa mshehereshaji wa harusi hiyo.
Pamoja na hayo Christina Matai pia ni Msanii wa maigizo, mf: Chai moto, Teke la mama, mama mkwe na nyingine nyingi. kwasasa Christina Matai anafanya maa ndalizi ya Albam nyingine.
Chai moto ni moja ya filamu ambayo Christina Matai ameshiriki kama jasmin |
Christina Matai akiwa nchini swaziland katika moja ya maeneo aliyowahi kwenda kufanya huduma.
christina matai akiwa na waimbaji wainjili wakiwa kwenye tamasha la marehemu fanuel sedekia
CHRISTINA MATAI akiimba kwa hisia katika huduma ya hakuna lisilowezekana BCIC TEMEKE
baadhi ya wanamusiki wa nyimbo za injili wakiwa kwenye uzindizi wa FLEM studio